Mkurugenzi wa Trickster, Sonobe Atsushi akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na uzinduzi wa shindano la kibiashara ambali litakuwa katika nchi tano za Afrika.
Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development Department(DMM) Bw.Alex Kapungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Trickster, Sonobe Atsushi.
Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development Department(DMM) Bw.Alex Kapungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Trickster, Sonobe Atsushi.
KAMPUNI ya Kijapani inayofanya shughuli zake nchini (Tricster) imeandaa shindano la wazo la biashara litakalozishirikisha nchi tano
za Afrika zikiwemo Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji
wa mashindano hayo kwa mwaka 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya
Afrika New Business Development Department(DMM) Bw.Alex Kapungu ambao ndio wadhamini wa shindano hilo ameeleza kuwa lengo
la shindano hilo ni kusaidia kuboresha
ujasiriamali katika bara la Afrika.
“Shindano
hili linafanyika kwa mara ya kwanza na hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali
na wale wanaotaka kuwa wajasiriamali kushiriki na baadaye kufanikisha wazo hilo
kiutendaji kwa kuwa biashara halisi”alisema Bw.Alex.
Aidha
ameongeza kuwa vigezo vya kushiriki shindano hilo ni mshiriki awe amefikisha
miaka 18 na kuendelea, awe anajua kuongea na kuandika lugha ya kiingereza na
kuwa na hati ya kusafiria.
Naye
Mkurugenzi wa Trickster Bw.Sonobe Atsushi amesema washindi watakaoingia nusu
fainali watapata fursa ya kutembelea
nchi ya japani ambapo mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu Dola elfu tano za kimarekani.
Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza na
kushiriki kwa wingi ili wapate fursa ya kuanzisha biashara kupitia mawazo
watakayoyatoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...