Na Albano Midelo,Songea

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama amezindua mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARSNA) unaogharimu shilingi bilioni 3.1 katika Kijiji cha Mpitimbi wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Waziri Mhagama amesema mradi huo unaotekelezwa na serikali katika mikoa ya Ruvuma na Lindi kwa unafadhiliwa na serikali ya Norway kupitia Shirika la NORAD na kwamba unatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Machi 2024 hadi Machi 2026.

Ameutaja mradi huo kuwa umelenga kuleta mabadiliko makubwa kwenye uzalishaji na uendelezaji wa biashara ya ufugaji Samaki na uzalishaji wa mwani kwa lengo la kuwawezesha wananchi kunufaika katika maeneo yao ufugaji Samaki na uzalishaji wa mwani.

Amesema serikali imekusudia kuendeleza kilimo na uvuvi katika mikoa ya Ruvuma,Lindi ili kupata mafanikio makubwa na kuongeza tija na kukabiliana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa vifaranga vyenye ubora na chakula cha Samaki.

“Kupitia mradi huu wazalishaji binafsi wa vifaranga vya samaki watajengewa uwezo katika uzalishaji wa vifaranga na wafugaji wa Samaki hususan vijana watajengewa uwezo wa kutengeneza chakula cha Samaki ’’,alisisitiza Mhagama.

Waziri Mhagama amesema tayari serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejenga shamba darasa la ufugaji wa samaki katika Kijiji cha Mpitimbi ambalo amesema litakuwa chachu kubwa katika ufugaji bora wa Samaki ambapo amewaomba wananchi hao kutumia shamba darasa hilo ili kuongeza tija katika ufugaji wa Samaki.

Ametoa rai kwa wakuu wa mikoa ya Ruvuma na Lindi ambako mradi huo unakwenda kutekelezwa kuhakikisha mradi unakwenda kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa ili kupata tija na thamani halisi ya fedha zitakazotumika.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Underson Mutatembwa ameutaja mradi wa ARSNA kuwa unataarajia kuzifikia kaya 5,000 za wakulima wadogo ikijumuisha wanawake asilimia 50 vijana asilimia 40 na makundi mengine asilimia 10.

Amesema mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 3.1 unatekelezwa katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Machi 2024 hadi Machi 2026 katika Halmashauri za Wilaya ya Songea na Mbinga mkoani Ruvuma na Halmashauri za Wilaya za Mtama na Ruangwa mkoani Lindi .

Amesema Tanzania imekuwa moja ya nchi tatu za Afrika zilizopata fursa ya kunufaika na utekelezaji wa mradi huu nchi nyingine amezitaja kuwa ni Msumbiji na Kenya na kwamba mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa program kubwa ya kuendeleza kilimo na uvuvi inayofadhiliwa na Shirika la IFAD inayotekelezwa katika mikoa 12 ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 150.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mwakilishi wa Mkurugenzi IFAD Afrika Mashariki na Kusini Jacquiline Machangu amesema IFAD imekuwa ikifanya kazi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo sekta ya kilimo hususan wakulima wadogo waliopo vijijini.

Amesema IFAD kupitia mradi wa ARSNA imelenga kuongeza mapato na kujenga uwezo kimaisha wafugaji wadogo katika maeneo matatu.

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni ongezeko la uzalishaji na ustahimilivu kwa wafugaji wadogo wa Samaki,kuongeza kwa fursa kwa wanawake na vijana kupitia ubunifu kwenye masoko na kuendeleza ujuzi na uundaji wa sera mpya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Alexander Mnyeti akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema Wizara hiyo itaendelea kutoa watalaam wa uvuvi ili kufanikisha mradi huo unakwenda kuzalisha Samaki wengi kwenye mabwawa ambao wana virutubisho muhimu.

Amesema Samaki wa mabwawa wanaweza kumaliza changamoto ya udumavu kwenye Mkoa wa Ruvuma ambapo hivi sasa udumavu umefikia asilimia 37 katika Mkoa wa Ruvuma , licha ya Mkoa huo kutajwa kuwa ni ghala la chakula nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameishukuru serikali kwa kuanza kutekeleza mradi huo mkubwa wa ufugaji Samaki katika Kijiji cha Mpitimbi.

Hata hivyo amesema serikali imekuwa inatekeleza miradi mikubwa katika jimbo la Peramiho ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nzito kutoka Likuyufusi hadi Mkenda mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Amesema mradi huo upo mbioni kuanza kutekelezwa serikali imetenga shilingi bilioni 74 kuanza kujenga lami kilometa 60 na kwamba serikali imetoa mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati mkoani Ruvuma.

Ameitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara ya lami nzito kilometa 66 kutoka Mbinga hadi Mbambabay kwa gharama ya shilingi bilioni 127,ujenzi wa bandari ya kimkakati ya Ndumbi kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni 12 na ukarabati wa uwanja wa ndege Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 37.










Nyumba ya kuishi familia mbili za walimu wa shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko iliyojengwa kwa fedha kutoka serikali kuu ambayo itawawezesha walimu kuishi karibu na eneo lao la kazi.
Mratibu elimu katika kata ya Mlingotimashariki wilayani Tunduru Erith Banga katikati, akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko Sabila Lipukila kushoto,kuhusu ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika shule hiyo yenye watoto zaidi ya 1,738 kati yao wanafunzi 43 ni wenye mahitaji maalum,kulia Mwalimu wa shule hiyo Ambilikile Mwandembo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko wilayani Tunduru Sabina Lipukila akiongea na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya elimu inayojengwa katika shule hiyo baada ya serikali kutoa zaidi ya Sh.milioni 300.

Na Mwandishi maalum, Tunduru
SERIKALI imetoa kiasi cha Sh.milioni 302 ili kuboresha mazingira na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi na walimu katika shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Sabina Lupukila amesema,kati ya fedha hizo Sh.milioni 246 zimetoka serikali kuu na Sh.milioni 56 zimetolewa na Halmashauri ya wilaya Tunduru.

Lipukila alisema,Sh.milioni 80 zimetumika kujenga bweni,Sh.milioni 50 kujenga nyumba moja ya walimu ya familia mbili,Sh.milioni 60 kujenga uzio na Sh.milioni 56 kwa ajili ya matundu 32 ya vyoo.

Aidha alieleza kuwa,Sh.milioni 56 zilizotolewa na Halmashauri ya wilaya Tunduru, Sh.milioni 41 zimetumika kumaliza ujenzi wa miradi hiyo iliyoanzishwa na serikali kuu na Sh.milioni 15 kwa ajili ya kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Alisema,bweni lina uwezo wa kuchukua watoto 80 na katika awamu ya kwanza litatumika kulala watoto wa kike wakati serikali ikiendelea na mchakato wa kujenga bweni lingine la watoto wa kiume.

Alisema, kwa sasa shule ya Tunduru Mchanganyiko ina wanafunzi 1,738 kati yao wanafunzi 43 ni wa elimu maalum kuanzia darasa la awali hadi la saba ambao wanatoka nyumbani na kwenda shule kila siku.

Lipukila alisema,ujenzi wa bweni hilo ni mpango wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa kuwajali watoto wenye mahitaji maalum na kuboresha mazingira ya elimu ili kuhamasisha watoto kupenda kusoma na wazazi kupeleka watoto wao shule kwa ajili kupata haki yao ya msingi.

Alisema,serikali inatambua umuhimu wa kuwa na mazingira mazuri ya kusoma ili kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kusoma bila vikwazo vyovyote kutokana na changamoto zao za kimaumbile.

Alisema, bweni hilo ni dawa itakayotibu watoto wote wenye mahitaji maalum waliopo katika wilaya ya Tunduru kutopenda kusoma na wengine kuacha shule kwani sasa kuna sehemu nzuri na rafiki itakayowawezesha kutimiza ndoto zao.

“watoto wenye ulemavu sio kwamba hawana ndoto,lakini changamoto kubwa imetokana na mazingira magumu kwa baadhi ya wazazi,natoa wito kwa wazazi na walezi wote wenye watoto wenye mahitaji maalum wawalete watoto wao kwenye shule hii”alisema.

Mratibu elimu kata ya Mlingoti Mashariki Erith Banda,ameishukuru serikali kujenga bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum na nyumba moja ya kuishi walimu.

Alisema,bweni hilo litamaliza adha kwa watoto wanaoishi mbali na shule kutumia muda mrefu kila siku kwenda kufuata masomo na kuepukana na changamoto mbalimbali za njiani.

Ambilikile Mwandembo anayefundisha watoto wenye ulamavu alisema,watoto hao wamegawanyika kwenye makundi matatu ambayo ni walemavu wa akili,ulemavu wa kusikia,mabubu,wenye uono hafifu na walemavu wa ngozi.

Alisema,watoto walemavu wanafundishika hivyo wazazi wachae tabia na kasumba ya kuwaficha watoto hao nyumbani,badala yake wawapeleke shule wakapate haki yao ya msingi.

Samia Shabani mwanafunzi wa darasa la saba alisema,bweni hilo ni muhimu sana kwa wenzao wenye ulemavu kwani sasa watapata muda mwingi wa kusoma kwa sababu wataishi shuleni.
Katika kupambana na udumavu mkoani Njombe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe imeendelea kufikisha ujumbe kwa jamii kwa namna mbalimbali na sasa ni zamu ya Bajaji kufikisha ujumbe huo kupitia Mabango.

Bwana Chrispin Kalinga kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema lengo la kuweka mabango hayo ni kufikisha ujumbe kwa jamii na Bajaji ni miongoni mwa chombo cha usafiri kinachotumiwa na watu wengi hivyo anaamini ujumbe huo utafika kwa jamii.

"Bajaji inatumiwa na makundi mbalimbali na rika tofuati tofauti na unafahamu hapa mjini Njombe na pale Makambako wananchi wanatumia sana usafiri wa Bajaji kwahiyo tunaamini kwa njia hii ujumbe utawafikia na adhma ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ni kuona udumavu unaisha ndani ya mkoa wetu" amesema Kalinga.

Baadhi ya Madereva Bajaji mjini Njombe wamesema hatua ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwashirikisha kupeleka ujumbe wa Lishe ni hatua nzuri kwani inaonesha serikali inatambua Bajaji ni moja ya sehemu inayohudumia watu wengi na itarahisisha ujumbe huo kufika kwa wananchi.

Kwasasa Kampeni ya Lishe mkoani Njombe inabebwa na kaulimbiu inayosema "Kujaza Tumbo Sio Lishe Jali Unachokula/ Unachomlisha" ikilenga kuhamasisha jamii kuzingatia lishe bora kutokana takwimu za matokeo ya awali ya utafiti wa hali ya afya nchini zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu Nchini (NBS) 2022 kuonesha mkoa huo bado una changamoto ya udumavu kwa asilimia 50.4, huku mkoa wa Iringa ukiongoza kwa asilimia 56.9.




Mkuu wa Progamu za Urithi wa Dunia wa Tume ya Taifa ya UNESCO Eric Kajiru akiwasilisha mada katika Semina ya wadau Maeneo ya Hifadhi za Asili ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani Dodoma


*Yataka wadau watumie fursa hiyo kabla ya vigezo havijabadilika

Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya UNESCO Tanzania imewataka wadau ambao wanataka kuziingiza maeneo yao katika orodha urithi wa dunia kuanza mchakato kabla ya 2027 kwani huenda taratibu zikabadilika na kuwa ngumu zaidi.

Akiwasilisha mada kwa wadau wa maeneo ya hifadhi za asili na utamaduni katika maadhimisho ya siku ya Siku Uridhi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani wa Dodoma, Mkuu wa programu za Urithi wa Dunia wa Tume Eric Kajiru amesema hivi sasa mchakato unaruhusu kuingiza hata sites 4 kwa wakati mmoja tofauti na utaratibu unaopendekezwa wa nchi kuwa na pendekezo la site moja kwa wakati mmoja.

Kajiru amesema Tanzania ina vivutio vingi vyenye sifa ya kuwa na hadhi hizo lkn kumekuwa na uzito katika kuanzisha mchakato jambo ambalo linalirudisha nyuma taifa.

Akizunguzia utayarishaji wa wasilisho la kutaka kutambulika na kuingizwa kwenye orodha ya urirhi wa dunia Kajiru amewataka wadau wahakikishe wanawashirikisha wadau wote wanaohusika ktk maendeleo ya maeneo yao ili kurahisisha mchakato na kuweka vipengele vya maangalizo iwapo eneo husika litahitajika ktk shughuli ingine.

Kuhusu mchango wa tume ya taifa kufanikisha hilo, Kajiru amesema tayari kuna baadhi ya maeneo ambayo yako katika hatua mbalimbali za kuandaa mawasilisho na kuwataka wadau wasisite kuwasiliana Tume pindi wanapohitaji muongozo na msaada unaolenga kufanikisha mchakato huo.

Ametoa mfano wa walipokuwa wakiingiza hifadhi ya Selous katika orodha mwaka 1982 watayarishaji walieleza kuwa serikali inampango wa kujenga Bwawa jambo ambalo lilisaidia kupitishwa kwa mradi huo kirahisi wakati ambao wanaharakati walitaka kuzuia lakini sasa umetekelezwa

Hivi sasa Tanzania ina maeneo ya Saba ya Uridhi Dunia ambazo ni Hifadhi ya Ngorongoro, Mji Mkongwe Zanzibar, Magofu ya Kilwa Songo Mnara na Kilwa Kisiwani, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Michoro ya asili ya Irangi Kondoa pamojà na Hifadhi ya Serengeti.
Mwandishi wa kitabu cha “And the Children Shall Lead Us”  Barry Childs (katikati) akionyesha nakala ya kitabu hicho katika  hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar e salaam hivi karibuni,wengine kwenye picha kushoto ni Mratibu wa mradi wa Africa Bridge  Kelvin Ngonyani  kulia ni mwandishi mwenza wa kitabu hicho, Philip Whiteley.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKA la kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu Africa Bridge limeweza kuwasaidia watoto 7,700 katika kata sita na vijiji 37 katika mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe kwa kuwasaidia na elimu, malazi na afya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa kitabu cha “And the Children shall Lead Us” mtunzi wa kitabu hicho Barry Childs alisema kwamba alirudi Tanzania baada ya miaka 35 na kuumizwa na hali aliyoikuta ya watu wa maeneo ya vijijini na kuamua kuanzisha shirika hilo la kutoa msaada.

“watu ambao wengi nilikua nao katika Mkoa wa Arusha kati ya 1944 hadi 1962 nilikuta hali zao bado ni duni na wengine walikuwa wameshapoteza maisha kutokana na umasikini wa kutupwa na nikaamua kuandika kitabu hiki ili kuleta mtazamo chanya wa kuweza kusaidia watu wa vijini hasa watoto,” alisema.

Alisema, muundo unaotumiwa na shirika hilo la Africa Bridge ni aina mbili kwanza kushirikisha watoto wenyewe na wazazi na pia kushirikisha jamii husika kupitia kwenye kamati za vijiji ili kuweza kusaidia katika malezi ya watoto kuanzia shule, nyumbani na kwenye jamii kwa ujumla.

Childs aliongeza kwamba kupitia mradi huo watoto wanajifunza shughuli za ujasiriamali kama vile kufuga ngo’mbe, kukamua maziwa na kuuza na upandaji na ulimaji wa zao la parachichi kwa ajili ya biashara,

Aliongeza kwamba utunzi wa kitabu hicho na uanzishwaji wa mradi huo unatokana na tafiti iliyofanywa na Chuo Kikuu Texas nchini Marekani kupitia kituo chao cha Utafiti cha Ray Marshall na kusema mfumo unaotumiwa na mradi utaleta matokeo chanya nchini Tanzania.

Kwa upande wake , Mratibu wa mradi huo, Kelvin Ngonyani alisema kwamba kitabu hicho chenye simulizi la kusisimua na kinacholenga kuwatoa watoto kwenye umasikini na kuwapa maarifa ya kilimo endelevu, ujasiriamali na kuboresha maisha yao hasa maeneo ya vijijini.

Aliongeza kwamba mfumo wa kuwahudumia watoto ni kwa kupitia kamati familia na jamii kwa kiwashirikisha viongozi wa kata, mitaa na vijiji ili kuweza kuleta ufanisi katika kutoa msaada wenye matokeo chanya kwa mtoto kuanzia malazi na elimu yao.

Mmoja wa wanufaika wa mradi huo , kutoka Mbeya wilaya ya Rungwe ni Sara Mosses (22) ambaye kwa sasa anasoma Chuo cha Rungemba Mafinga na anachukua Stashada ya Maendeleo ya jamii ambaye alisema....mie ni mmoja wa wanaufaika na mradi huu kwa kusomeshwa kupitia zao la parachichi kuanzia shule ya msingi, sekondari na kwa sasa nachukua stashada ya Maendeleo ya jamii na nataka kurudi kuendelea kuhudumia jamii yangu hasa watoto ambao wako kwenye mazingira magumu hapa nchini,”

Mtunzi wa kitabu hiki kinachoitwa “And the Children Shall Lead Us” (Na Watoto Watatuongoza) Barry Childs, ambaye alikulia Tanzania na baadaye alikwenda kusoma Shahada ya Sayansi katika Saikolojia katika Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal Afrika kusini.

Childs alifanya kazi kwa miaka 17 katika kampuni ya Exxon na baadaye alikuwa Mkurugenzi wa Masomo katika Maabara ya Abbott. Baada ya miaka 35 akiwa nje ya nchi, Childs ameamua kurudi Tanzania ili kuendeleza ndoto yake ya kuwatoa watoto kwenye umaskini.


Sehemu ya kitabu chake inasema kwamba aliporudi nchini alikuta watu wakipambana na umasikini na athari za ugonjwa wa Ukimwi, hivyo aliamua kujipanga akiwa kwenye shirika la Abbot 2000 na kuanzisha mradi unaoitwa ‘Africa Bridge’ kusaidia watoto wa Kitanzania.

Kitabu hiki chenye kurasa 168 kimechapishwa kwa lengo la kushirikisha jamii kwa jumla juu ya mafanikio ya mradi wa Africa Bridge katika kuleta uzoefu katika utafiti ya kitaaluma na kuzidisha uelewa kwa jamii juu ya uwezo wake mkubwa wa kuwainua watoto walio hatarini zaidi kutoka kwenye umasikini.

Childs aliamua kuanzisha mradi wa Africa Bridge ili kuionyesha dunia namna bora ya kutumia rasiliamali zilizopo kama ardhi na kilimo ili kuweza kumwinua mtoto wa Kitanzania na jamii kwa jumla kuondokana na umasikini.

“And the Children Shall Lead Us” kinaelezea jinsi mradi wa Africa Bridge unavyofanya kazi, ulivyotokea na kutekelezwa, na yale yaliyofunzwa katika miaka 23 ya uendeshaji wake.

Childs, ambaye ni mwanzilishi wa Africa Bridge, aliishi miaka yake ya utotoni Tanzania na alimua kurudi baadaye kujitolea kusaidia nchi yake ya asili.

Kitabu hiki, kinachokusudiwa kuwa somo pendekezi katika Sayansi za Jamii, kinaelezea simulizi la kuvutia la mradi wa Africa Bridge, shirika la jamii la pekee, ambalo limeendeleza mfano wa kujitegemea unaokubalika wa kuinua jamii za watu wa vijijini Afrika kutoka katika umaskini uliopitiliza.

Mwanzilishi wake Bw Childs anaamini kwamba ili kubadilisha maisha ya watoto walio hatarini, mtiririko salama wa mapato ni muhimu kwa kuwaendeleza, kupata elimu, na kutoa fursa halisi za kuwawezesha kufikia malengo yao.

Africa Bridge ilianzisha vyama vya ushirika vya kilimo na kamati za watoto na za kuwainua wanawake wa vijijini kwa kuwawezesha kwa vitendo ili kuzalisha mapato endelevu huku wakikidhi mahitaji ya jamii.


Mwanzilishi wa Mradi wa Africa Bridge na mtunzi wa Kitabu cha ‘And the Chidren Shall Lead Us, chenye simulizi ya kuwatoa watoto kwenye umasikini na kuwapa maarifa ya kilimo endelevu, kuboresha maisha yao, Barry Childs (katikati) akikata utepe kuzindua kitabu hicho kupitia mradi wa Africa Bridge nchini, hafla ya uzinduzi huo imefanyika jijini Dar es Salam.
Mwandishi wa kitabu cha “And the Children Shall Lead Us,  Barry Childs akielezea historia ya maisha yake nchini Tanzania na sababu ya kuandika  kitabu hicho.
Mwandishi wa kitabu cha “And the Children Shall Lead Us”  Barry Childs akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi wa mradi wa Africa Bridge nchini,Baraka Mtunga wakati wa hafla  hiyo.
Baadhi ya washiriki  wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.


JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya jana kushuhudia mitanange kibao ikipigwa. Leo hii kipute hicho kitaendelea kama kawaida timu kibao leo zipo uwanjani kusaka pointi tatu kujiweka sawa kabla msimu huu haujaisha. Meridianbet tayari wamekuwekea ODDDS za kibabe na machaguo zaidi ya 1000.

Pale ligi kuu ya Uingereza, EPL leo hii kutakuwa na mechi tatu kali Chelsea takuwa Stamford Bridge kucheza dhidi ya West Ham United ikiwa ni Derby huku mechi ya mkondo wa kwanza The Blues walichapika. Meridianbet wamempa Pochettino nafasi kubwa ya kushinda mechi hii kwa ODDS 1.59 kwa 4.60. Suka mkeka wako hapa.

Wakati huo huo Aston Villa baada ya kutoa sare mchezo wake uliopita, atakuwa ugenini kupepetana dhidi ya Brighton ambao wapo nafasi ya 13 kwenye ligi na tofauti ya pointi kati yao ikiwa ni 23 tuu. Villa wanataka kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao. Mechi hii imepewa ODDS 2.60 kwa 2.50. Jisajili hapa.

Ukiachana na mechi ndugu mteja kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Mechi ya mwisho Uingereza leo hii ni ya Liverpool ambao watakuwa pale Anfield kukiwasha dhidi ya Spurs majira ya saa 12:30 jioni. Klopp na vijana wake wametoka kutoa sare mechi iliyopita na Tottenham amepoteza. Je leo hii nani kuibuka na ushindi? Ingia meridianbet ubashiri sasa mechi hii ambayo imepewa ODDS 1.43 kwa 5.88.

Kule Italia, SERIE A pia kuna mechi za maana kabisa Hellas Verona atakuwa mwenyeji wa ACF Fiorentina ambaye yupo nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi na mwenyeji wake akiwa nafasi ya 15. Mara ya mwisho kukutana Fiorentina alishinda. Je leo hii mwenyeji anaweza lipa kisais?. Mechi hii ina ODDS 3.23 kwa 2.27. Suka jamvi lako hapa.

Saa 1:00 AC Milan atamualika Genoa ambapo ukiingia ndani ya mwridianbet mechi hii imepewa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000. Milan ya Pioli wapo nafasi ya pili na mgeni wake yupo nafasi ya 12. Je nani kukupatia pesa Jumapili ya leo uanze Jumatatu yako vizuri?. Ingia meridianbet na ubashiri sasa.

Juventus baada ya kutoa sare mechi yake iliyopita, leo hii atakuwa ugenini kukiwasha dhidi ya AS Roma huku mechi ya kwanza Allegri na vijana wake walishinda. Roma amepewa ODDS 2.84 kwa 2.60 kushinda mechi hii. Tofauti ya pointi kati yao ni 6 tuu. Bashiri hapa.

Tukipaa hadi Hispania sasa kule LALIGA, baada ya kumpata bingwa wa ligi hiyo sasa ni zamu ya timu nyingine kusaka nafasi nzuri RC Celta Vigo uso kwa uso dhidi ya Villarreal ambao wapo nafasi ya 9 kwenye ligi. Vigo yupo nafasi mbaya kwenye ligi na mechi ya mkondo wa kwanza alipoteza. Je atapindua meza leo?. ODDS KUBWA zipo mechi hii. Tengeneza jamvi lako sasa.

Sevilla ataumana dhidi ya Granada majira ya saa 4:00 usiku huku mwenyeji yeye akitoa sare mechi yake iliyopita na mgeni akishinda. Mwenyeji ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu kwa ODDS 1.64 kwa 5.09. Wewe unampa nani pesa yako leo akupe mkwanja?. Beti hapa.

Naye Rayo Vallecano atajipima tena dhidi ya UD Almeria ambao ndio vibonde wa ligi. Mwenyeji yupo nafasi ya 15 huku mechi ya kwanza walipokutana alishinda. Mechi hii imepewa ODDS 1.57 kwa 5.48. Je nani kuondoka kifua mbele?. Tengeneza jamvi lako hapa wakati huu.

Ujerumani pia BUNDESLIGA kitawaka kama kawaida Union Berlin atakuwa mwenyeji wa VFL Bochum huku timu hizi zikiwa zimefatana sana kwenye msimamo wa ligi yani nafasi ya 14 na 15 huku pia zikilingana pointi. Mechi ya mkondo wa kwanza mgeni alishinda, Je leo hii Berlin atafanya maajabu?. Mechi hii imepewa ODDS 1.96 kwa 3.87. Bashiri kijanja hapa.

Saa 12:30 jioni Eintracht Frankfurt atakipiga dhidi ya Bayer Leverkusen ambaye tayari ni bingwa wa ligi hiyo. Mechi ya kwanza Alonso na vijana wake walishinda. Je leo hii kwa ODDS ya 2.11 kwa 3.23 wanaweza kushinda pia?. Suka mkeka wako hapa.

Huku FC Heidenheim wao watakuwa na kibarua cha kukabiliana na FSV Mainz ambapo tofauti yao ni pointi 9 pekee. Mwenyeji yupo nafasi ya 11 na mgeni yupo nafasi ya 16 huku mechi ya kwanza mgeni alipasuka. Ingia meridianbet na ubeti sasa.
Na Mwandishi Wetu – Songea

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA) katika kijiji cha Mpitimbi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma Tarehe 4 Mei 2024.

Mradi huo wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA) unaoenda kutekelezwa katika Wilaya nne za Mikoa ya Ruvuma na Lindi, na kulenga katika kunufaisha kaya elfu Moja (1000) katika Wilaya za Songea vijijini, Mbinga Mkoani Ruvuma, Ruhangwa na Mtama Mkoani Lindi, ambapo pamoja na mambo mengine Familia na jamii hizo zinaenda kuinua hali ya maisha kwa kuongeza kipato na kuimalisha Lishe.

Akiongea katika uzinduzi wa mradi huo,Waziri Mhagama alisema Mpitimbi imebahatika kuanza na mradi huu, na kwakuwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula lakini, una changamoto ya udumavu,”Na ndiyo maana Serikali imeleta mradi huu ambao utatumia takribani zaidi ya shilingi Bilioni tatu nukta moja, katika maeneo tuliyojipangia, ambao ni sehemu ndogo tuu ya Programu kubwa ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi, Tumebahatika kuanza na mradi huu unaofadhiliwa na ubalozi wa Norway Nchini hivyo ni wakati mzuri wa Wilaya zitakazonufaika kuweza kujikimu kimapato na kiafya.” Alisema.

Aliendelea kusema kuwa, kwa kuwa hali ya udumavu inaleta changamoto ya afya ya akili ni fursa sasa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kuendelea kuboresha afya, kupitia lishe ya viumbe maji na hasa Samaki.

Waziri Mhagama aliushukuru ubalozi wa Norway kupitia shirika lake la NORAD kuleta mradi huo mkoani Ruvuma, “Leo Tunazindua Shamba Darasa Ambalo linaenda kuchagiza maendeleo ya tabianzuri ya biashara na matumizi ya lishebora kupitia samaki wanaofugwa kwenye mabwawa, na miradi itakayofanywa kwenye baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.” Alisisitiza.

Alibainisha kuwa, Kupitia bwawa kubwa la Asili lililopo Mpitimbi ni wakati sahihi sasa wa kuimarishwa kwa bwawa hilo na kuanza kwa ufugaji mkubwa wa Samaki “Tunatamani kuona kuwa Bwawa hilo lenye ukubwa wa hekari 17.4 linaendelezwa na kuwa shamba Darasa.” Alisema

Awali, Waziri Mhagama Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa, kupeleka Miradi mingi ya Maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa alisema, kupitia mradi huo unaoenda kutekelezwa kwa miaka miwili,Tanzania imekuwa Miongoni mwa nchi tatu za Afrika kupata bahati ya kunufaika na Mradi huo, zikiwemo nchi za Kenya na Msumbiji.

Aliendelea kusema kuwa, mradi huo wa kuendeleza Lishe na ufugaji endelevu wa viumbemaji na ukulima wa mwani kwa wakulima wadogo unatekelezwa katika mikoa kumi na moja ya Tanzani Bara pamoja visiwa vya unguja na Pemba.

Akiongea katika ghafla hiyo muwakilishi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo nchini (IFAD) Bi. JacquiIine Machangu Motcho aamesema, IFAD imekuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika nyanja na sekta zinazolenga, kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya kilimo hususani Wakulima wadogo wadogo hasa wale walio vijijini.

Na aliendelea kusema kuwa, Shirika hilo limeendelea pia kuyapa kipaumbele maeneo hayo ikiwa na dhamira ya kuinua na kuboresha sekta ya Kilimo, Mazao, Mifugo na Uvuvi ili kufikia uzalishaji wa juu ulio endelevu na wenye faida kibishara, unaoleta ukuaji wa pamoja kiuchumi na Taifa zima kwa ujumla.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Bi JacquiIine alisema Kupitia Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi, IFAD imepokea ufadhili-ruzuku(grant) kwa mradi wa ARNSA kutoka Ubalozi wa Norway, unaolenga kupunguza umaskini na kuboresha lishe kupitia shughuli za Ufugaji wa Samaki wenye tija na ustahimilivu kutoka kwa wazalishaji/wafugaji wadogo. Dhamira yake ya kimaendeleo inalenga kuongeza mapato, kujenga ustahimilivu na kuwajengea uwezo kimaisha wafugaji wadogo wa samaki walio vijijini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (aliyeinama) akiweka mbegu ya Samaki katika moja ya Bwawa, wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024

*Yataka wadau watumie fursa hiyo kabla ya vigezo havijabadilika



Na Mwandishi Wetu

Tume ya taifa ya UNESCO imewataka wadau ambao wanataka kuziingiza maeneo yao katika orodha urithi wa dunia kuanza mchakato kabla ya 2027 kwani huenda taratibu zikabadilika na kuwa ngumu zaidi.

Akiwasilisha mada kwa wadau wa maeneo ya hifadhi za asili na utamaduni katika maadhimisho ya siku ya Siku Uridhi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani wa Dodoma, Mkuu wa programu za Urithi wa Dunia wa Tume Eric Kajiru amesema hivi sasa mchakato unaruhusu kuingiza hata sites 4 kwa wakati mmoja tofauti na utaratibu unaopendekezwa wa nchi kuwa na pendekezo la site moja kwa wakati mmoja.

Kajiru amesema Tanzania ina vivutio vingi vyenye sifa ya kuwa na hadhi hizo lkn kumekuwa na uzito katika kuanzisha mchakato jambo ambalo linalirudisha nyuma taifa.

Akizunguzia utayarishaji wa wasilisho la kutaka kutambulika na kuingizwa kwenye orodha ya urirhi wa dunia Kajiru amewataka wadau wahakikishe wanawashirikisha wadau wote wanaohusika ktk maendeleo ya maeneo yao ili kurahisisha mchakato na kuweka vipengele vya maangalizo iwapo eneo husika litahitajika ktk shughuli ingine.

Kuhusu mchango wa tume ya taifa kufanikisha hilo, Kajiru amesema tayari kuna baadhi ya maeneo ambayo yako katika hatua mbalimbali za kuandaa mawasilisho na kuwataka wadau wasisite kuwasiliana Tume pindi wanapohitaji muongozo na msaada unaolenga kufanikisha mchakato huo.

Ametoa mfano wa walipokuwa wakiingiza hifadhi ya Selous katika orodha mwaka 1982 watayarishaji walieleza kuwa serikali inampango wa kujenga Bwawa jambo ambalo lilisaidia kupitishwa kwa mradi huo kirahisi wakati ambao wanaharakati walitaka kuzuia lakini sasa umetekelezwa

Hivi sasa Tanzania ina maeneo ya Saba ya Uridhi Dunia ambazo ni Hifadhi ya Ngorongoro, Mji Mkongwe Zanzibar, Magofu ya Kilwa Songo Mnara na Kilwa Kisiwani, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Michoro ya asili ya Irangi Kondoa pamojà na Hifadhi ya Serengeti.
Mkuu wa Progamu za Urithi wa Dunia wa Tume ya Taifa ya UNESCO Eric Kajiru akiwasilisha mada katika Semina ya wadau Maeneo ya Hifadhi za Asili ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani Dodoma


Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Na Alex Sonna-KASULU VIJIJINI
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeanza kutekeleza agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kufunga mitungi katika vikosi vyake lengo likiwa ni kutunza na kulinda mazingira.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema hayo mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Brigedia Jenerali Mabena amesema katika kutekeleza kwa vitendo agizo la hilo,JKT kwa kushirikiana na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) walizunguka katika vikosi vyote vya JKT nchini ili kuangalia namna bora ya kuweka miundombinu.

Amesema vikosi vingine vinaendelea kutengeneza miundombinu kama ilivyokuwa imeshauriwa na ile kamati ambayo imehusisha REA na wataalamu kutoka JKT.

"Sasa kwa kuwa wapo na wanaendelea ile kamati maalum waliweza kupita kwenye vikosi vyote na kuweza kuangalia miundombinu na kutoa maelekezo na ushauri namna ya kufanya.

"Ni pamoja na kuandaa majiko na kusimika mitungi mikubwa ya gesi huku wakiendelea kusubiri Mpango wa REA ili kuhakikisha mazingira yanakuwa salama,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Amesema kikosi cha 825 Mtabila na chenyewe kipo katika hatua za utekelezaji.

Brigedia Jenerali Mabena amekipongeza kikosi hicho kwa hatua hiyo ambayo wameifanya kwani ni maagizo ya Serikali na kuwa wadau wa matumizi ya kupikia.

Amesema JKT wanawahudumia wadau wengi kwani vikosi vya kujenga Taifa kwa mwaka mmoja wanakuwa na vijana wa kwa mujibu wa sheria wanaofikia laki moja.

"Utaona vijana hawa wanahitaji kupata chakula kwa kuwa JKT sisi ni wadau wakubwa na mazingira yetu yanaendelea kuwa salama tunayalinda kwa namna yoyote.

"Na katika kuyalinda kwanza kabisa hatukati miti na tumekuja na kampeni kabambe ya tunapanda miti katika maeneo yetu ya vikosi lakini kwa kutumia nguvu kazi kwa kupanda katika Wilaya na Halmashauri zinazotuzunguka kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani,"amesema Mkuu huyo wa tawi JKT

Kwa upande wake Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,amesema zoezi hilo lilianzia mara baada ya maelekezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Ofisi ya Muungano na Mazingira kupitia Makao Makuu ya JKT

Amesema wao kama kikosi walipokea maelekezo hayo na kwa sababu wanawahudumia watu wengi na wao waliamua kulitekeleza.
"Hili jiko la gesi tumetumia gharama zote kwa vyanzo vya ndani.Lakini pia ni sehemu kama shamba darasa kujifunza na jinsi ya kutunza mazingira,"amesema

Amesema kama kikosi wanaendelea na jitihada za kupanda miti ambapo mpaka sasa wamepanda miti 13,000 na 1000 ya matunda.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akisoma ujumbe mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiangalia majiko na Mitungi mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

 

MERIDIANBET Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahia mchezo uliochochewa na mandhari maarufu zaidi. Unaweza kufikiri ni nini? Bila shaka, ni kuhusu Misri ya kale. Pata bonasi zenye nguvu ambazo mafarao wanakuletea.

Cobra Queen ama Malkia wa Nyoka ni Kasino Mtandaoni kutoka kwa muuzaji Red Tiger. Mchezo unuletea ugeuzaji wa alama zinazoshiriki katika mfululizo wa kushinda kuwa kadi za porini. Zaidi ya hayo, utafurahia mizunguko ya bure.

Mchezo huu wa Kasino mtandaoni ndani ya Meridianbet una nguzo tano zilizopangwa katika safu tatu na ina mistari 10 ya malipo. Ili kupata ushindi wowote, unahitaji ufananishe alama tatu au zaidi kwenye mstari wa malipo.

Isipokuwa kwa sheria hii ni alama ya Kleopatra. Pia itakuletea ushindi na alama mbili katika mfululizo wa kushinda. Mchanganyiko wote wa kushinda katika mchezo huu wa Kasino Mtandaoni unahesabiwa kutoka nguzo ya kushoto kwenda nguzo ya kulia.

Ndani ya kasino mtandaoni hii, kuna vitufe vya kuongeza na kupunguza ambavyo unaweza kuweka thamani ya dau lako kwa kila mzunguko.

Pia, kuna chaguo la Kucheza Kiotomatiki, ambacho unaweza kuwasha unapotaka. Kupitia chaguo hili unaweza kuweka hadi mizunguko/Spin 100. Kabla ya kuanza kazi hii, weka kikomo kuhusu hasara iliyopatikana wakati wa Kucheza Kiotomatiki.

Ikiwa unafurahia mchezo wa kiasi kidogo zaidi, tuna suluhisho kwa hilo pia. Weka haraka kwa kubonyeza kisanduku kilichoandikwa Turbo.

Alama za Ushindi Kwenye Kasino Mtandaoni ya Cobra Queen (Malkia wa Nyoka)

Linapokuja kwa alama zinazolipa kidogo, katika mchezo huu utaona alama za kadi za kawaida: 10, J, Q, K na A. Inayolipa zaidi miongoni mwao ni alama ya A. Alama tano za aina hii katika mfululizo wa kushinda hulipa mara 10 ya dau.

Jicho la Misri na msalaba huleta nguvu ya kulipa hata kubwa zaidi. Ikiwa utafanana na alama tano za aina hii katika mchanganyiko wa kushinda, utashinda mara 25 ya dau.

Inafuata nondo ya skarabu, ambayo huleta nguvu ya kulipa isiyo ya kawaida. Ikiwa utafanana na alama tano za aina hii katika mchanganyiko wa kushinda utashinda mara 40 ya dau lako.

Alama yenye thamani zaidi ya mchezo ni malkia wa Misri, Kleopatra. Ikiwa utafanana na alama tano za aina hii kwenye mstari wa malipo utashinda mara 100 ya dau lako.

Bonasi Katika Mchezo Huu wa Kasino Mtandaoni.
Bonasi za Kasino Unapopata ushindi, baada ya malipo, alama ya mwisho katika mfululizo wa kushinda itageuka kuwa porini. Joka linaakumulisha thamani ya ushindi ndani yake na linabaki katika nafasi yake wakati wa spin inayofuata.

Ikiwa litapatikana katika mfululizo wa kushinda wakati wa spin inayofuata, pia linabaki katika nafasi yake. Itaondolewa kutoka kwenye nguzo na spin ya kwanza isiyoshinda.

Inawezekana kwa majoka kadhaa kupatikana kwenye nguzo wakati ule ule. Kazi yao kuu ni kubadilisha alama zote, isipokuwa mwanaskati, na kuwasaidia kuunda mchanganyiko wa kushinda.

Mwanaskati anawakilishwa na mafarao na anaonekana kwenye nguzo ya kwanza, ya tatu, na ya tano. Alama tatu za aina hii kwenye nguzo zinaleta moja kwa moja raundi 10 za bure.

Ikiwa porini itaonekana wakati wa raundi za bure, inabaki katika nafasi yake hadi mwisho wa mchezo wa bonasi na inakusanya thamani ya ushindi ambayo inashiriki.

Unapojaza nguzo moja na alama za porini, unashinda raundi mbili za bure zaidi.

RTP ya ushindi wkenye Kasino Mtandaoni hii ya Cobra Queen ni 96.02%. Malipo ya juu ni mara 2,000 ya dau ulilocheza.

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni Lakini pia unaweza kubashiri soka kwa ODDS KUBWA na machaguo 1000+. Jisajili na Cheza.

Na Mwandishi wetu, Simanjiro

DIWANI wa Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel Lesenga Maridadi amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2 na kufanikisha miradi ya maendeleo kwenye eneo hilo.

Lesenga ameyasema hayo kwenye mkutano wa wakazi wa Kijiji cha Loiborsiret wa kueleza na kusoma utekelezaji wa ilani ya CCM na kueleza mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusikiliza kero na changamoto za jamii ya eneo hilo.

Diwani huyo amesema Rais Samia amefanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata yake ya Loiborsiret hivyo ni jukumu la jamii ya eneo hilo kumuunga mkono pindi ukifika muda wa uchaguzi mwaka 2025.

"Rais Samia hoyee tunamshukuru kwa kutumwagia miradi mingi ya maendeleo kwenye kata yetu ya Loiborsiret na tunamuahidi kuwa naye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho kwa kumpa kura zote za ndiyo," amesema Lesenga.

Amesema hadi hivi sasa kwenye vijiji vyote vitatu vya kata ya Loiborsiret vya Kimotorok, Narakauo na Loiborsoit, vimepata umeme na daraja la Loiborsiret limejengwa.

"Kituo cha afya kata ya Loiborsiret ujenzi unaendelea, jengo la mama na mtoto tayari, ukarabati wa bwawa la Narakauo limekamilika na maji yapo ya kutosha," amesema Maridadi.

Diwani huyo amesema barabara ya kutoka Korongoni kwenda Loiborsiret hadi kitongoji cha Irmang'wa kwa sasa inapitika kwa nyakati zote.

"Uanzishwaji wa shule shikizi katika maeneo ya kata ikiwemo shule shikizi iliyokamilika ya Oltepeleki kijiji cha Loiborsiret, shule shikizi ya Noomoton kijiji cha Narakauo," amesema Maridadi.

Amesema pia umefanyika ujenzi wa shule shikizi mtoni kijiji cha Narakauo, shule shikizi Noomokon kijiji cha Narakauo na shule shikizi ya Olmoti iliyopo Kijiji cha Loiborsiret," amesema.

Amesema pia umefanyika ujenzi wa madarasa mapya matatu yaliokamikika katika shule ya msingi Loiborsiret, ukamilishaji wa madarasa matatu shule ya msingi Kangala na ujenzi wa maabara shule ya sekondari Loiborsiret.

"Pia ujenzi wa computer lab shule ya sekondari Loiborsiret na ununuzi wa computer kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Loiborsiret," amesema Diwani huyo.

Amesema hivi sasa kuna ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kimotorok ambao bado unaendelea.

Mmoja kati ya wakazi wa kijiji cha Loiborsiret, Kalai Mollel amesema wameona jitihada za Diwani wao katika kuwasomea ili wapate maendeleo hivyo anapaswa kuungwa mkono.

Mkazi mwingine Leronjo Lembaji amesema hadi hivi sasa wakazi wa eneo hilo wameona jitihada kubwa zilizofanywa na Diwani wao.




NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa amesema Chama hicho kitaendelea kuwa mtetezi na mwangalizi wa Wananchi wote.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kada wa CCM ambaye ni Mkurugenzi mstaafu idara ya umwagiliaji Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt.Ramadhan Aseid Ramadhan huko nyumbani kwake Fuoni.

Dkt.Dimwa,amesema lengo la ziara yake hiyo ni kumtembelea ili kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara zake za kuwatembelea makada,wazee na wananchi kwa ujumla.

Alieleza kuwa ziara hizo zinaendeleza utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi wa kuweka daraja huru la mahusiano mema baina ya Chama na Wananchi bila kujali tofauti za kidini,kisiasa na kikabila.

"Kila nikikutana na wazee na makada wakongwe waliotumia nguvu na muda wao kuitumikia nchi yetu kwa uadilifu nafurahi sana kwani napata ushauri,mbinu na nasaha nzuri za kunisaidia katika masuala ya utendaji na kuwatumikia kwa ufanisi zaidi wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla.

Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kushinda katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025 ili tuendelee kuongoza nchi kwa uadilifu na ufanisi mkubwa kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazoendana na mahitaji yao ya sasa kiuchumi,kijamii na kimaendeleo",alisema Dkt.Dimwa.

Naye Mkurugenzi mstaafu idara ya umwagiliaji Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt.Ramadhan Aseid Ramadhan,amemshukru Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Dimwa kwa kumjali na kumtembelea kwa dhamira ya kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya Kijamii.

Dkt.Aseid,amempongeza kwa dhati Naibu Katibu Mkuu Dkt.Dimwa kwa utendaji wake unaoleta ufanisi na mabadiliko mkubwa ya kiutendaji ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na kada wa CCM ambaye pia ni mkurugenzi mstaafu idara ya umwagiliaji Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt.Ramadhan Aseid Ramadhan nyumbani kwake Fuoni Zanzibar.



Top News