Kikosi Cha Taifa Stars
Kikosi cha Rwanda
Makapteni wa timu zote mbili wakisabahiana mbele ya waamuzi waliochezesha mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Mrisho Ngasa (kulia) akimtoka beki wa timu ya Rwanda 'Amavubi' Nghabo Albert katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Jerry Tegete akijaribu kupiga shuti wakati wa mchezo.
Kipa wa Amavubi, Ndayishimiye jeanluc akijarribu kuokoa kiki iliyopigwa na Mrisho Ngasa bila ya mafanikio.
Beki wa timu ya taifa ya Rwanda, Nghabo Albert akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Stars, Juma Jabu katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) ulliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1
Benchi la ufindi la Taifa Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Jooooob true true! Hata Rwanda wajemeni? Afu eti uwanja wa omu? Safari ni mureeefu true true! Duh. Embu angalia ilo likisimo (lilivyoduwaa). Uyu na utaalamu wake wa mabua wote huo bado ajuhi kuwa angelimteua Kaseja angelikuwa anasmaili nau! Ha ha haaa. Eli kamkataba kake kamesharegea! He heee!

    Dayasipora

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2010

    Mdharau mwiba.

    Hakuna uwiano wa soka na ukubwa wa nchi. Chezea hengine siyo Rwanda.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2010

    hahahahah sawa sawa anony hapo juu jamaa anaonekana ni mvivu wa kufkiria saana afu kune soka kila kitu cha wezekana daika 90 lazima ue tayari kwa kila kitu.kuidharau rwanda hata mfaransa au mjinga yeyeto ka ww hapo juu dayasipora endeleeni sie tunasonga kama kawa na mtalijua jiji na wajinga wenzio ww dayasipoara.jamaani ka rwanda ketu kametiotahidi safari hii ngoja tusubirie kagame cup a.k.a cecafa tuone inakuaje

    mdau kigali makazi boksini kusaka chake

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2010

    Taafa Stars nikama kifaranga cha kuku kilichohaidiwa nyonyo, toka enzi za kichwa cha mwendawazimu maksi hazimo,
    Wachezaji wamejaa misifa tu,pamoja na viongozi wao Wanazidi tu kuchanika na Pesa za Uwanja na Wafadhili, hata tovuti hakuna.
    Niwakati wa kusimamia kidete Soccer Academy sasa sio hao mashaibu.
    Mdau,
    Barcelona

    ReplyDelete
  5. KUIFUNGA SOMALIA NCHI ISIYO NA LIGI YOYOTE WALA SERIKALI AKAONA NI KIPIMO TOSHA, AKAJISIFU KUWA NITAONDOKA TZ NA KUWAACHIA ZAWADI KUBWA, NAYO NI UBINGWA WA CAN. SASA SIJUWI YUHALI GANI? MAMBO NDO HAYO JAHAZI LISHAANZA KUTOTA

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2010

    Wadau mi nadhani sisi watanzania ni walaini sanaaaa (Nimejaribu kutumia neno baridi)sijui tunaweza kujivunia nini! Hatuna dila tupo tuuu mladi kumekucha baraka ya kuchekeana tuu! Inauma sanaaa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2010

    We Maximo zimo kweli? utamuwekaje Mussa Hassan Mgosi (Mussa Magoli) benchi halafu umuingize kipindi cha pili. Unategemea magoli yataingiaje?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2010

    tuachane na hao wachezaji wa uswazi wavuta bangi, tutafute vipaji vijijini, vijana wa copa cocacola tuwatumie tutapata timu nzuri. hawa wameshindikana, hata kama tutamleta mourinho kuwafundisha hawa atachemsha tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2010

    Wamejitahidi ila tatizo kubwa kuna siasa ambazo hazifai kwa kuendeleza soka. Upangaji wa timu mara nyingine uanaleta mashaka kama vile kuna wau wanasema fulani lazima acheze. Kama siyo hivyo, kwa kocha makini hawezi kumwanzisha benchi Mgosi, mkumbuke kuwa ktk nchi zinazojua soka mfungaji bora ni muhimu kwa taifa na hata watu wa nchi nyingine wanapotaka kucheza na timu wanapitia mchezaji mmoja mmoja wa timu pinzani kuona profile zao, sasa nashangaa kwa TZ sijui kocha nalijua hili ama anajitahidi tu kupanga kufurahisha watu, imefikia wakati soka liendeshwe kisayansi zaidi na kiukweli kuliko kuingiza sisa ambazo hazina maana, katika hili tusubiri kocha nayekuja ambaye hatokumbwa na sisa hizi na ubishi ambao hauendelezi soka. Mpeni Papic muone atakavyofanya, anajua soka ndiyo maana mara zote ingawa yuko Yanga hatosita kusifia kizuri cha timu pinzani, huyu anjua soka na si majungu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2010

    Hivi jezi za stars zimebadilika? Naona katka mechi na Rwanda jezi zina nembo ya adidas.Hawakuvaa za kawaida kama zilizovaliwa na Ngorongoro Boys Ijumaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2010

    Hivi jezi za stars zimebadilika? Naona katka mechi na Rwanda jezi zina nembo ya adidas.Hawakuvaa za kawaida kama zilizovaliwa na Ngorongoro Boys Ijumaa

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2010

    jabu si mshambuliaji ni mlinzi wa pembeni

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2010

    FRANKLY I LOVE TAIFA STARS LAKINI HIZI JEZI HAZINA MSHIKO!!!

    PLEASE TFF HUYO MZAMINI APELEKE HIZO RANGI MNAZO TAKA ZA JEZI ZA TAIFA KWA WATAALAMU WA KUDESIGN WALOBOBEA WASEZIINI JEZI ZA MAANA. HIZI JEZI HAZIVUTII, HALAFU TUACHE USIMBA NA UYANGA, JEZI ZA NJANO NI MZURI KWA FAIDA MOJA ZINAFANYA WACHEZAJI WAONEKANE, SISI WEUSI THEN TUNAVAA RANGI YA BLUE ILIYOFIFIA NA NYEUSI..CHECK MSAJIGWA HAPO???? KISA WASHIBIKI WA SIMBA WATACHUKIA??? HILI NI TAIFA SIYO SIMBA NA YANGA, AU JIE TFF HAMJUI KUWA RANGI INAYONG'ARA UWANJANI INASAIDIA KULETA USHINDI. BRAZIL WANAJUWA HILI, NDIYO MAANA HAWAVAI JEZI ZA KIJANI AMBAYO IMETAWALA KATIKA BENDERA YAO, WANAVAA NJANO ILI WAONANE VIZURI....NA WANAVUTIA UWANJANI

    CHITU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...